Waathirika wa Fidia ya Uhalifu


Chini ni baadhi ya taarifa za msingi kuhusu fidia kwa waathirika wa uhalifu na uhakiki. Haitolewi kama ushauri wa kisheria. Kama ungependa ushauri na msaada kwa waathirika wa madai ya uhalifu, tupigie kwa 1800 684 055 ili kufanya miadi kuzungumza na mwanasheria

Nini maana ya Fidia ya Waathirika wa Uhalifu?

Fidia ya waathirika wa uhalifu ni msaada wa kipesa kwa waathirika wa matendo ya vurugu ambayo hutokea katika Mkoa wa Kaskazini.
Fidia ya waathirika wa uhalifu hulipwa chini ya mpango wa Fidia ya Waathirika wa Uhalifu.Waathirika wa matendo ya vurugu ni kama:

  • Shambulio
  • Shambulio la kijinsia
  • Unyanyasaji wa majumbani

Mtu yeyote ambaye alipata jeraha (ya kimwili, kifedha * kisaikolojia) kama matokeo ya uhalifu anaweza kuomba kwa ajili ya fidia ya waathirika wa uhalifu. Unaweza kuomba fidia hata kama hakuna mtu aliyeshtakiwa kwa uhalifu. Ni muhimu kuripoti uhalifu kwa polisi. kiasi cha fidia kinachopokelewa (kama kipo) kitategemea kiwango cha majeraha na hasara ya kuteswa kwa muathirika

Nani anaweza kuomba Fidia ya Kuathirika na Uhalifu?

 Unaweza kuomba kama:

  • Ni muathirika wa matendo ya vurugu na umeumia, au umekubwa na hasara ya kifedha, kwa sababu ya maumivu.
  • Ni muathirika wa matendo ya vurugu, hata kama hutaumia maumivu mengine (e.g. shambulio la kijinsia)
  • Wewe ni mtu wa karibu na mtu aliyekufa kutokana na matendo ya vurugu au umekubwa na hasara ya kifedha.
  • Watu wanaoumia kwa sababu wameshuhudia matendo ya vurugu, kujaribu kuokoa mtu mwingine au kujaribu kuzuia matendo ya vurugu anaweza pia kupata fidia ya uathirika wa uhalifu.

Lini naweza kufanya maombi?

Ni lazima kufanya maombi ndani ya miaka 2 kutoka wakati vurugu zilipotokea. Maombi yanaweza kukubaliwa baada ya miaka 2 kama kuna sababu nzuri kwa nini hayakuweza kuwakilishwa kwa muda. Zungumza na mwanasheria kama unadhani unawakilisha maombi nje ya muda.

Jinsi gani naweza kufanya maombi?

Unaweza kuomba fidia ya uathirika wa uhalifu kwa kujaza fomu iliyoko hapa .

Unaweza pia kuomba nakala ya fomu kwa kupiga

1800 460 363.

 Jinsi gani Huduma ya Sheria ya Wanawake inavyoweza kusaidia?

Tunaweza kutoa ushauri kuhusu fidia ya waathirika wa uhalifu na kukujulisha kama unaweza ukastahiki. Kama una madai halali, tunaweza kukusaidia kujaza fomu na kutoa uwakilishi unaoendelea na msaada kupitia mchakato madai. Tupigie kwa

1800 684 055 ili kufanya miadi kuzungumza na mwanasheria, au fika kutuona katika ofisi yetu ya Alice Springs office mda wowote.

Ushauri na msaada

Waathirika wa matendo ya vurugu na ndugu zao na marafiki wa karibu wanastahili kwa ushauri wa bure.Kwa habari zaidi, wasiliana na Anglicare NT kwa 1800 898 500.

Familia ya watu waliokufa ikiwa ni matokeo ya matendo ya vurugu wanaweza kuomba fidia ya gharama za mazishi na/au msaada wa pesa.

 

Habari zaidi na msaada

Swahili
Language
Audio
Play
Play
Play
Play
The Central Australian Women’s Legal Service Thank the 'Law Society Public Purposes Trust' for Supporting the Language Translations on this Site