Unyanyasaji wa Majumbani na Familia

Unyanyasaji wa majumbani na familia unaweza kutokea kwa mtu yeyote…

Kama wewe au mtu unayemjua yuko kwenye hatari, piga 000 na uliza polisi.

Unaweza kuzungmza na mshauri aliyebobea kwenye masuala ya unyanyasaji wa majumbani na familia masaa 24, siku 7 za wiki kwa kuita 1800Huduma ya Taifa ya Ushauri ya Kuheshimu Utu na Unyanyasaji wa Majumbani (Respect National Sexual Assault and Domestic Violence Counselling Service) kwa 1800 737 732.

Washauri pia wapo kwenye  mtandao kwenye http://www.1800respect.org.au

Nini maana ya Unyanyasaji wa Majumbani na Familia?

Unyanyasaji wa Majumbani na Familia hutokea wakati mtu mmoja katika uhusiano atumiapo vurugu au tabia ya matusi kumtawala mtu mwingine.

Unyanyasaji wa majumbani na familia unajumuisha:

 • Unyanyasaji wa kimwili unaojumuisha kupiga, kupiga ngumi, kupiga kofi, kuvuta nywele, kupiga fimbo
 • Kuharibu mali, ikijumuisha kuumiza au kuua wanyama
 • Vitisho, kumufanya mtu ajione mdogo
 • Kudhibiti tabia (kwa mfano, kumukataza mtu kuona familia na marafiki)
 • Unyanyasaji, ikijumuisha kwa njia ya simu, ujumbe wa simu, barua, kwenye Facebook na vyombo vingine vya habari
 • Kunyemelea – kufuata, kutazama au kusubiri mtu
 • Unyanyasaji wa kiuchumi (kwa mfano, kuchukua pesa, kushikilia pesa, kumkatalia mtu asifanye kazi)

Unyanyasaji wa majumbani na familia hautokei tu kwa wanaume na wanawake. Unatokea kwenye uhusiano mwingi wa karibu, kama:

 • Uhusiano wa Kuishi Pamoja (watu wanaoishi pamoja kama mke na mme lakini wakiwa hawajaoana)
 • Uhusiano wa jinsia moja
 • Ndugu – ikijumuisha akina mama, baba, ndugu wa kuzaliwa, shangazi, wajomba, babu na bibi, binamu, watoto, watoto wa kambo, wazazi wa kambo, wakwe na ndugu wa jamii ya Wazawa
 • Ndugu ambao au wamekuwa wakifanya mepenzi, hata kama kidogo na hata kama uhusiano wao sio wa kimapenzi
 • Wapenzi wa zamani

Utoaji taarifa wa Lazima

Katika Mkoa wa Kasikazini, watu wazima wote wanatakiwa na sheria kuripoti vurugu za majumbani na familia polisi kama wanafikiri mtu ana au kuna uwezekano wa kuteseka kimwili kwa sababu ya vurugu.

Ripoti lazima ifanyike kwenye polisi kwa kuita 131 444.  Katika hali ya hatari, ita 000.

Ni kosa la jinai kutoripoti kama unanaamini kwamba mtu ana au kuna uwezekano wa kuteseka sana kimwili

Habari zaidi kuhusi utoaji taarifa wa lazima unapatikana kwenyetovuti  ya Kusimamisha Vurugu za Famia ya Serikali ya Australia ya Kasikazini (Northern Territory Government’s Stop Family Violence)

Jinsi gani Huduma ya Sheria ya Wanawake ya Australia ya Kati inavyosaidia?

Kama unahangaika na vurugu za majumbani na familia, unaweza kuomba kuwekwa utaratibu maalum dhidi ya mkosaji. Utaratibu wa unyanyasaji wa majumbani ni utaratibu ambao mahakama inaamuru mkosaji kukaa mbali nawe na/au kusimamisha kukudhuru.

CAWLS ni huduma ya sheria ya bure na siri kwa wanawake wote wa Australia ya kati.

Tunaweza kutoa ushauri kuhusu utaratibu wa unyanyasaji wa majumbani na jinsi unavyofanya kazi, na kukusaidia jinsi ya kuomba Mahakamani ili kupata amri ya unyanyasaji wa majumbani.

Piga 1800 684 055  ili kupata miadi, au fika kutuona kwenye ofisi zetu za Alice Springs office mda wowote.

Tunaweza kusaidia na rufaa ili kusaidia mashirika kuhakikisha kuwa uko salama.

 Habari zaidi na msaada

 • Malazi ya wanawake ya Alice Springs : panasaidia wanawake na watoto wanaohangaika na vurugu za nyumbani na familia, ikiwa ni pamoja na malazi ya dharura. Simu. 8952 6075 au temebelea tovuti ili kupata habari zaidi http://asws.org.au
 • 1800 HESHIMA( RESPECT): huduma ya taifa ya ushauri ya unyanyasaji wa kijinsia na vurugu za familia. Piga 1800 737 732 masaa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki. Au tembelea tovuti http://www.1800respect.org.au
 • Vijitabu vya habari kuhusu kupata amri juu ya unyanyasaji wa nyumbani: kwa watu wanaohitaji usalama  na kwa washtakiwa  (inatolewa na Serikali ya Mkoa wa Kaskazini) (tafadhali wasiliana nasi kama ungependa kupata kijitabu katika lugha yako)
 • Tovuti ya Kusimamisha Unyanyasaji ndani ya Familia http://www.stopfamilyviolence.nt.gov.au: habari kuhusu kutoa taarifa juu ya kutoa taarifa kwa lazima za unyanyasaji wa nyumbani.

 

Swahili
Language
Audio
Play
Play
Play
Play
CAWLS thanks the Law Society Public Purposes Trust for supporting the language translations on this site.