Ulinzi wa Mtoto

Kama mtoto wako au mtoto katika familia yako amechukuliwa katika huduma na Idara ya Watoto na Familia (pia inajulikana kama ‘DCF’, au ‘Ustawi’), au kama ukipata karatasi yoyote kutoka Idara ya Watoto na Familia, ni muhimu kuzungumza na mwanasheria mara moja. Tupigie kwa 1800 684 055 kufanya miadi ili kuonana na mwanasheria. Tunaweza kuzungumza na wewe pia kwenye simu kama huwezi kuja kwenye ofisi yetu, na tutakutuma kwa wanasheria wengine kama hatuwezi kukusaidia

 Nini maana ya sheria ya ulinzi wa mtoto? Jinsi gani inafanya kazi?

 Mkoa wa Kaskazini una sheria ya kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa, afya na wako salama kutokana na madhara. Idara ya Watoto na Familia (DCF) ina wajibu wa kuhakikisha watoto ni salama na wenye afya.Mkoa wa Kaskazini ‘utoaji taarifa wa lazima’. Hii ina maana kwamba mtu mzima yeyote analazimika kutoa taarifa kwa DCF au polisi kama anafikiri kwamba mtoto anatunzwa vibaya, au amewahi kutunzwa vibaya huko nyuma. Hii ni pamoja na kimwili na kihisia, kingono na kupuuzwa.Wakati DCF au polisi ilipata ripoti kuhusu mtoto anayetendewa vibaya, DCF inatathmini ripoti. Wakati mwingine DCF inaweza kuamua kwamba kila kitu ni sawa. Mara nyingine DCF inaweza kuzungumza na wazazi na familia ili kujua njia za kuwasaidia ili kuwatunza watoto na kuwafanya wawe salama.Kama DCF wana wasiwasi hasa kuhusu mtoto na wanadhani kuwa si salama kwa mtoto kukaa mahali ambapo wanaishi, DCF itaondoa mtoto na kuwatunza chini ya uangalizi wao. Wakati mwingine, hii itakuwa tu kwa muda mfupi ili DCF iweze kuchunguza kitu kinachoendelea.Mara nyingine hii itakuwa kwa muda mrefu – miezi michache au mwaka au wakati mwingine mda mrefu zaidi. Kama ni mbaya sana hii inaweza kuwa hata mtoto atakapofikisha miaka 18. Wakati DCF inataka kumtunza mtoto kwa muda mrefu, italazimika kuomba ruhusa mahakama.

Mkataba na DCF

Wafanyakazi wa DCF wakati mwingine wanauliza wazazi na familia kama wanakubaliana watoto wao kwenye uangalizi wao kwa muda mfupi. Hii inaitwa Mkataba wa Ulinzi wa Mda Mfupi. Hii inaweza kuwa hivyo ili wazazi waweze kuwa na muda bila watoto wa kutatua matatizo waliyonayo au kusaidia mtotot mgojwa ili apone.  Kama DCF ikikuuliza kusaini makubaliano kuhusu watoto wako, ni vizuri kuzungumza na mwanasheria kwanza, hasa kama huna uhakika ni nini mkataba unazungumzia. Unaweza kuzungumza na mwanasheria kwa kupiga 1800 684 055

Amri za Mahakama

Kama DCF ikiuliza Mahakama juu ya amri kuhusu watoto wako, ni muhimu kwamba wewe kuzungumza na mwanasheria mara moja – tupigie simu kwa 1800 684 055 au njoo kuona nasi haraka kama unaweza. DCF lazima ikupe nakala ya maombi inayoonyesha siku ambayo kesi yako itakuwa mahakamani.DCF lazima iithibitishie Mahakama kwamba watoto wako wanahitaji uangalizi, na kuonyesha Mahakama mipango jinsi watoto wako watakavyotuzwa baada kuchukuliwa katika huduma yao, na jinsi watakavyokuwa na mawasiliano na wewe.Unaweza kusaidiwa na wakili kwa kuzungumza na DCF kuhusu mpango huu, na kukusaidia kufanya makubaliano na DCF kuhusu kuona watoto wako wakati wakiwa chini ya ulezi wao. Kama hutakwenda Mahakama siku hiyo ambapo maombi yanafanyika, Hakimu anaweza kutoa amri juu ya watoto wao hata kama wewe hauko pale. Ni vizuri kujaribu kuzungumza na mwanasheria kabla ya siku hiyo ya mahakama, lakini haijalishi hata kama hujafanya hivyo – Bado hujachelewa kuzungumza na mwanasheria na kuwaomba msaada.

Jinsi gani Huduma ya Sheria ya Wanawake inavyoweza kusaidia?

Tunaweza kutoa ushauri kuhusu jinsi sheria za ulinzi wa mtoto zinavyofanya kazi, na kueleza kile kinachotokea kwenye suala yako. Tunaweza pia kusaidia kwa kuzungumza na DCF na kuielezea DCF historia ya upande wako. Huhitaji kusubiri mpaka mambo yako mahakamani ndio uzungumze na wanasheria. Njoo kwetu haraka mara tu baada ya kupata karatasi kutoka DCF, au wakati wowote ukiwa na wasiwasi juu ya kile kinachotokea. Mara nyingi ni bora kuzungumza na sisi mapema, baada ya hapo tunaweza kukusaidia wakati mwingine kutatua mambo kabla ya kwenda Mahakama. Kama suala lako likienda Mahakama, tunaweza kukuwakilisha katika Mahakama na kuhakikisha kuwa unakuwa na la kusema kuhusu nini kinatokea kwa watoto wako. Tupigie kwa 1800 684 055 ili kufanya miadi ya kuzungumza na mwanasheria

Swahili
Language
Audio
Play
Play
Play
Play
The Central Australian Women’s Legal Service Thank the 'Law Society Public Purposes Trust' for Supporting the Language Translations on this Site