Sheria za Familia na Watoto

Chini ni baadhi ya taarifa za msingi kuhusu jinsi mfumo wa sheria za familia zinafanya kazi kuhusu mipango ya uzazi wakati watu wanapoachana. Hazitolewi ushauri wa kisheria. Kama unafikiria kuachana au umeshaachana, unatakiwa kuomba ushauri wa kisheria kabla ya kufanya maamuzi kuhusu kitu cha kufanya. Tupigia kwa 1800 684 055 ili kupata miadi ya kuongea na mwanasheria.

Kutengana na watoto – jinsi gani inafanya kazi?

Wakati unapotengana, mpenzi wako wa zamani atahitaji kufanya maamuzi ya muhimu kuhusu malezi ya watoto ya mbeleni.

Sheria ya Familia ya 1975 ni sheria inayoonyesha kitu kinachotokea kwa familia zilizoachana kuhusu kutengana, mipango ya malazi, mali na utashi wa matengenezo.

Sheria inasema ni muhimu kwa watoto kuwa uhusiano mzuri na kila mzazi na watu wengine ambao ni muhimu katika maisha yao (kama mababu na mabibi), kama ni kwa ajri ya faida ya watoto na labda kama inawaweka watoto katika hasara ya kuumizwa.

Sheria inalazimisha wazazi kufanya juhudi za kumaanisha kutatua matatizo ya ulezi bila kwenda mahakani. Wazazi wanatakiwa kufikia makubaliano kuhusu mipangilio ya watoto wao na jinsi ya kupata huduma ya kutatua matatizo ya kifamilia, kama vile upatanishi, ili kuwasaidia kufikia makubaliano.

Unyanyasaji wa majumbani katika uhusiano unaweza kuathiri jisni sheria inavyofanya kazi. Ni muhimu kujulisha mwanasheria wako kama unahangaika, au umepatwa na vurugu za majumbani.

Kufanya mpangilio baada ya kuachana

Baada ya kuachana, ni muhimu kuangalia mpangilio wa kuishi wa watoto wako, ikijumuisha kiasi cha mda utakaotumiwa, na jinsi mtakavyowasiliana, ninyi kama wazazi. Ni muhimu kuangalia jinsi maamuzi ya mbeleni yatakavyotatuliwa kuhusu watoto.

Unaweza kuzungumza na lawyer ili kupata ushauri na msaada kuhusu mipangilio mnayoweza kuifanya.  Wewe na mpenzi wako wa zamani mnaweza pia kuhudhuria suluhisho la mizozo ya familia kama vile upatanisho.

Suluhisho la Mizozo ya Familia na Upatanishi

Usuluhishi ni mchakato ambapo wewe na mpenzi wako wa zamani mnaweza kuja pamoja kujadili mipango kwa ajili ya watoto wenu. Hufanyika katika uwepo wa mtu anayejitegemea na asiyependelea aitwaye ‘mpatanishi’. Mpatanishi hawezi kukushauri au kufanya maamuzi kwa ajili yenu – kazi yao ni kuwasaidia wazazi kufikia makubaliano, kwa pamoja.

Wakati mukifikia makubaliano amabayo wote wawili mnayafurahia, yanaweza kuwa kumbukumbu kama ‘mpango wa uzazi’ au ‘ridhaa ya maagizo’. Unapaswa kupata ushauri wa kisheria kabla ya kusaini mpango wa uzazi au maagizo ya ridhaa.

 

Mipango ya Uzazi

Mpango wa uzazi ni mkataba ulioandikwa ambao unaweka mipango ya uzazi kwa ajili ya watoto. Inafanywa na kukubaliwa na pande zote mbili, hivyo hakuna haja ya kwenda mahakamani. Mpango wa uzazi haufugwi na sheria.

 

Ridhaa ya Maagizo

Ridhaa ya Maagizo ni mkataba ulioandikwa ambao hupitishwa na Mahakama. Una nguvu kisheria sawa na amri inayotolewa baada ya kesi kusikilizwa Mahakama. Wewe na mpenzi wako wa zamani munaweza kuomba ridhaa ya maagizo bila ya kwenda Mahakamani.

 

Kwenda mahakani

Kama makubaliano hayawezi kufikiwa, unaweza kuuliza Mahakama kuamua kuhusu mipango yenu ya uzazi

Kabla ya kwenda Mahakamani, wewe na mpenzi wako wa zamani mnatakiwa kuhudhuria suluhisho la mizozo ya famila, kama vile upatanishi. Mahakama haitakubali maombi yenu isipokuwa kama muna cheti kutoka kwa mpatanishi.  Uhitaji huu wakati mwingine unaweza kuondolewa ikiwa kuna wasiwasi unaohusiana na vurugu za familia au unyanyasaji wa watoto.
Jinsi gani Huduma ya Sheria ya Wanawake ya Australia ya Kati inavyosaidia?

Tunaweza kutoa ushauri kuhusu mipango ya uzazi, idhini ya utekelezaji na kwenda mahakamani, pamoja na maswala mengine ya sheria za familia (kama maswala ya kuuza nyumba).

CAWLS ni huduma ya sheria ya bure na siri kwa wanawake wote wa Australia ya kati.

Tunatoa vikao vya ushauri wa bure kwa wanawake wote. Tunaweza kutoa misaada ya kuendelea na uwakilishi katika baadhi ya kesi.

Ikiwa muhimu, tunaweza kusaidia katika rufaa kwa huduma zingine za sheria na mashirika ya kusaidia.


Habari zaidi na msaada

  • Mahakama ya Sheria ya Familia  ina habari nyingi kuhusu familia zilizotengana, ikijumuisha vijitabu Ndoa, Familia na Kutengana. Simu. 1300 352 000 au tembelea tovuti http://www.familylawcourts.gov.au
  • Relationships Australia: huduma ya kusaidia masuala ya ndoa, ikijumuisha huduma ya ushauri kwa wanandoa walioachana/waliotengana, na Huduma ya Usuluhishi wa Masuala ya Familia. Simu 1300 364 277 au tembelea tovuti http://www.nt.relationships.org.au
  • Laini ya Ushauri wa Uhusiano wa Familia : 1800 050 321. Msaada kwa familia zilizoathirika na uhusiano au matatizo ya kutengana.
  • Uhusiano wa Familia wa kwenye Mtandao : Taarifa na ushauri kuhusu masuala ya uhusiano wa familia kwa familia zote (iwe pamoja au zilizotengana), ikiwa ni pamoja na taarifa kuhusu huduma ambazo zinaweza kuwasaidia kusimamia masuala ya uhusiano, ikiwa ni pamoja na kukubaliana juu ya mipango sahihi kwa watoto baada ya kutengana.

http://www.familyrelationships.gov.au/Pages/default.aspx

Swahili
Language
Audio
Play
Play
Play
Play
CAWLS thanks the Law Society Public Purposes Trust for supporting the language translations on this site.