Sheria za Familia na Mali

Hapa chini ni baadhi ya taarifa za msingi kuhusu jinsi mfumo wa sheria ya familia inahusika na mali wakati watu wakiachana. Hazitolewi kama ushauri wa kisheria. Kama unafikiria kuachana au umeshatangana, unapaswa kutafuta ushauri wa kisheria kabla ya kufanya uamuzi kuhusu nini cha kufanya. Piga kwa 1800 684 055 kufanya miadi ili uzungumze na mwanasheria.

Kutengana na mali – inafanya kazi namna gani?

Wakati ukiachana, wewe na mpenzi wako wa zamani utahitaji kufanya maamuzi juu ya matumizi ya pesa, mali na vitu unavyovimiliki. Sheria ya Familia ya 1975 ni sheria inayoeleza kitu gani kinatokea kwa familia zinazotengana baada ya kuachana, mali na matengenezo ya utashi .Wakati wa kuamua jinsi ya kugawanya mali, sheria inaonekana katika kila kitu ambacho wanandoa wanamiliki na kupata (ikijumuisha akiba ya uzeeni na madeni), na kugawanya hizi kulingana na kile kinachoonekana kuwa haki. Katika Australia, sheria haiangalii ni vyanzo vya kuachana au nani ana makosa. Kugawana nyumba sio kuangalia nani ana haki na yupi hana haki.Unyanyasaji ndani ya uhusiano unaweza kuathiri jinsi sheria inavyofanya kazi. Ni muhimu basi mwanasheria wako ajue kama unahangaika, au kupatwa na unyanyasaji wa majumbani.

Ni wakati gani naweza kuomba msaada wa kugawana mali?

Pale unapoachana, ni muhimu kupata ushauri wa kisheria kuhusu haki zako, na kupata fununu jinsi sheria inavyosema kuhusiana na kugawana mali sawa. Kama ukiachana, una miezi 12 kutoka siku mlipoachana katika kuomba amri juu ya mali zenu. Kama uko kwenye uhusiano wa kuishi pamoja tu, ni lazima uombe ndani ya miaka 2 toka tarehe mlipoachana.

Kitu gani kinajumuishwa katika ‘mali’?

Kwa lengo la kugawana mali, mali inajumuisha nyumba, pesa (pesa katika akaunti za banki), miradi, bima, urithi, hisa, akiba ya uzeeni, mapambo, magari na mali zingine. Wote ninyi na mpenzi wako wa zamani lazima kutoa taarifa yote na sahihi ya uwezo wa kipesa.

Kufanya mapatano

Wewe na mpenzi wako wa zamani mnaweza kukubaliana juu ya jinsi ya kugawana mali na fedha. Makubaliano yanaweza kufanyika katika amri ya mahakama yanayoitwa kibali cha idhini. Wakati unaomba kwa ajiri ya kibali cha idhini, Mahakama itakubali tu kutoa amri kama itakuwa ni ‘Haki na usawa’– lazima iwe sawa kwa pande zote.Unaweza pia kuingia katika Mkataba Fedha halisi. Mkataba huu hautunzwi na Mahakama lakini lazima uzingatia sheria ili ukubarike kisheria..

Mahakama inaamua namna gani kwamba nani apate hiki?

Sheria imeweka hatua nne za kufuata za kusaidia kuamua jinsi ya kugawana mali:

  1. Tambua mali zote katika uhusiano.
  2. Angalia mchango wa kila mmoja katika uhusiano. Hii inajumuisha mchango wa kipesa katika mali, pia mchango kama mtunzaji wa nyumba na mzazi.
  3. Zingatia vigezo vingine vilivyoko katika sheria, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa mapato siku za mbeleni, kiasi cha mda wa uhusiano, ulezi wa watoto.
  4. Jadili jinsi ya kugawana mali, ukihakikisha kuwa ni kwa haki na sawa katika mazingira husika.

Jinsi gani Huduma ya Sheria ya Wanawake ya Australia ya Kati inavyosaidia?

Tunaweza kutoa ushauri kuhusu kugawana mali pamoja na masuala mengine ya familia (kama mipango ya malezi ya watoto)

CAWLS ni huduma ya sheria ya bure na siri kwa wanawake wote wa Australia ya kati.

Tunatoa vikao vya ushauri wa bure kwa wanawake wote. Tunaweza kutoa misaada ya kuendelea na uwakilishi katika baadhi ya kesi.

Ikiwa muhimu, tunaweza kusaidia katika rufaa kwa huduma zingine za sheria na mashirika ya kusaidia.Tugigie kwa1800 684 055 ili kufanya miadi ya kuonana na mwanasheria.


Habari zaidi na msaada

http://www.familylawcourts.gov.au

  • Relationships Australia: huduma ya kusaidia masuala ya ndoa, ikijumuisha huduma ya ushauri kwa wanandoa walioachana/waliotengana, na Huduma ya Usuluhishi wa Masuala ya Familia. Simu 1300 364 277 au tembelea tovuti

http://www.nt.relationships.org.au

  • Laini ya Ushauri wa Uhusiano wa Familia : 1800 050 321. Msaada kwa familia zilizoathirika na uhusiano au matatizo ya kutengana.
  • Uhusiano wa Familia wa kwenye Mtandao : Taarifa na ushauri kuhusu masuala ya uhusiano wa familia kwa familia zote (iwe pamoja au zilizotengana), ikiwa ni pamoja na taarifa kuhusu huduma ambazo zinaweza kuwasaidia kusimamia masuala ya uhusiano, ikiwa ni pamoja na kukubaliana juu ya mipango sahihi kwa watoto baada ya kutengana.

http://www.familyrelationships.gov.au/Pages/default.aspx

Swahili
Language
Audio
Play
Play
Play
Play
The Central Australian Women’s Legal Service Thank the 'Law Society Public Purposes Trust' for Supporting the Language Translations on this Site