Ajira & Ubaguzi

CAWLS inaweza kusaidia wanawake wenye matatizo yanayoendana na kazi.
Tunaweza kusaidia na vitu kama:

  • Malipo na mazingira ya kazi
  • Uonevu kazini
  • Unyanyasaji wa kijinsia
  • Kujeruhiwa kazini na fidia ya mfanyakazi
  • Ubaguzi
  • Kufukuzwa bila haki

 

MUHIMU: kama umefukuzwa kutoka kazini na hujafanya chochote kibaya (kufukuzwa bila sababu) unahitaji kuzungumza na mtu mara moja – una siku 14 tu kuwakilisha malalamiko.  Tupigie kwa 1800 684 055 kufanya miada ili kuzungumza na mwanasheria.  Hakikisha unatwambia kuwa ni haraka na kwa unahitaji kuonana na mtu mara moja.

 

Kituo cha Wanawake Wanaofanya Kazi wa Mkoa wa Kaskazini (NTWWC) kinatoa ushauri wa bure na wa siri kwa wanawake kuhusu masuala yanayohusiana na kazi. NTWWC ina vijitabu mbalimbali vizuri na kumbukumbu kuhusu masuala yanayoendana na kazi. Hivi ni mahali pazuri pa kuanzia kujifunza zaidi kuhusu matatizo, na kitu unachoweza kukifanya.  Unaweza kupata vijitabu hivyo na machapisho kwenye tovuti http://www.ntwwc.com.au.

Kama ukitaka ushauri na msaada kuhusu masuala yanayoendana na kazi, piga 1800 684 055 kufanya miada kuongea na mwanasheria kwenye Huduma ya Sheria ya Wnawake wa Australia ya kati au pigia Kituo cha Wanawake Wnaofanya Kazi cha NT kwa 1800 817 055.

Swahili
Language
Audio
Play
Play
Play
Play
CAWLS thanks the Law Society Public Purposes Trust for supporting the language translations on this site.