Kitu tunachofanya

CAWLS inatoa ushauri wa kisheria bure kwa wanawake wote wa Australia ya kati.

CAWLS inatoa:

 • Kusaidia unyanyasaji wa majumbani bila miadi na huduma ya waathirika wa uhalifu
 • Vikao vya ushauri bure kwa kufanya miadi
 • Miadi ya jioni

Tunaweza kukusaidia na:

 • kupata, tofauti au kupinga amri ya unyanyasaji wa majumbani
 • sheria za matatizo ya familia – watoto, mali, matengenezo na msaada wa wtoto
 • fidia – waathirika wa uhalifu, ajari za magari, ajari za kazini
 • ulinzi wa mtoto
 • ubaguzi
 • ajira na kufukuzwa kazi
 • mikopo na masuala ya madeni
 • upangaji

Huduma za kuwakilishwa za kisheria zinapatikana katika baadhi ya kesi.

Kama unafikiri unahitaji ushauri wa kisheria, tafadhali wasiliana nasi  to make an appointment.

Tunatoa pia elimu ya sheria kwa jamii, kuwa na  huduma za nje  na kufanya  sheria  zifanye kazi.


Huduma ya Mwanasheria wa Zamu wa Unyanyasaji wa Nyumbani

Mwanasheria kutoka CAWLS huhudhuria Mahakama ya Alice Springs kila Jumatatu asubuhi kusaidia wanawake masuala mbalimbali yahusuyo unyanyasaji wa majumbani.


Huduma za Nje

CAWLS husafiri kusaidia wanawake wanaoishi maeneo ya vijijini katika Australia ya kati.

Tunasafiri mara kwa mara kwenda Ti Tree, Ltyentye Apurte (Santa Teresa) na Tennant Creek.
Katika Tennant Creek, tunapatikana kwenye Ofisi za Northern Territory Legal Aid Commission 168 Patterson Street (karibu na Juu kwenye Mji).  Tunapatikana kwa miada ya ushauri na kusaidia wanawake wenye matatizo ya unyanyasaji wa nyumbani kwenye Mahakama (Kila Jumatano Asubuhi).
Ili kujua zaidi kuhusu utembeleaji wa jamii vijijini, au kama unapenda tutembelee jamii yako, tupigie kwa 1800 684 055.
Tunaweza pia kutoa ushauri na msaada kwa njia ya simu kwa wanawake wa vijijini. Simu 1800 684 055
Kurekebisha Sheria

CAWLS inahusika katika marekebisho ya sheria zinazoendana na masuala yanayowathiri wanawake katika Mkoa wa Kasikazini. Tunafanya hivi kwa kuwasilisha katika maoni ya bunge na ubadilishi wa sheria, kuhusika katika mashirika yanayowakilisha jamii, kukutana na wanasiasa na wawakilishi wa serikali na kutoa maoni kwenye vyombo vya habari.

Swahili
Language
Audio
Play
Play
Play
Play
Play
Play
Play
Play
Play
Play
Play
The Central Australian Women’s Legal Service Thank the 'Law Society Public Purposes Trust' for Supporting the Language Translations on this Site